Takriban watu 53 wamefariki wakati basi lililokuwa likivuka daraja katika Jiji la Guatemala lilipogongana na magari mengine kadhaa na kisha kutumbukia kwenye korongo.
Maafisa usalama wa Serikali wamesema, Basi hilo liliangukia katika eneo ambalo ni gumu kufikika na kuzama kwenye mto wa maji taka, huku mizigo na vitu kibinafsi vy wasafiri vikitawanyika kwenye kingo za maji.
Idadi ya waliofariki ilitarajiwa kuongezeka kutokana na ajali hiyo, huku Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Umma, ambayo ilitoa idadi ya waliofariki katika taarifa, ikisema inachunguza ajali hiyo iliyotokea mwendo wa saa 4:30 asubuhi ya Februari 10, 2025.
Msemaji wa Idara ya Zimamoto ya jiji la Guatemala, Carlos Hernández alisema Dereva wa basi hilo alipoteza udhibiti wa gari kwa sababu ya hitilafu ya mitambo na kuyagongana na magari mengine mawili.