Ajali 1,641 zaua Wanaume 1,189 Tanzania

Serikali imesema katika kipindi cha Januari Mosi hadi Desemba 13, 2023 jumla ya ajali 1,641 zimetokea barabarani na kusababisha vifo vya watu 1,550 huku wanaume wakiwa 1,189, ambao ni sawa na asilimia 76.7.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni ambapo amesema madereva 1,226 walifikishwa mahakamani na madereva 2,596 walifungiwa leseni kutokana na makosa mbalimbali.

Aidha, katika majeruhi 2,562 wa ajali hizo, wanaume waliojeruhiwa ni 1,721 sawa na asilimia 67 huku idadi ya majeruhi wanawake wakiwa 841, ambao ni sawa na asilimia 33

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *