Ahukumiwa maisha kwa kosa la kumlawiti mwanae

Mahakama Ya Wilaya ya Shinyanga Imemuhukumu Kifungo Cha Maisha Jela Mkazi Wa Ngokolo Abel John Haule Mwenye Umri Wa Miaka 37 Kwa Kosa La Kumlawiti Mtoto Wake Wa Miaka 11.

Akitoa Hukumu Hiyo Leo Agosti 3, 2023 Hakimu Mfawidhi Wa Mahakama Ya Wilaya Shinyanga Yusuph Abdllah Zahoro Ameeleza Kuwa Abel Amekuwa Akimfanyia Kitendo Hicho Mtoto Wake Kwa Muda Wa Miaka Miwili Na Kutoa Vitisho Vikali Endapo Atatoa Taarifa.

Aidha Zahoro Ameongeza Kuwa Kitendo Hicho Kimepelekea Madhara Kadhaa Ya Afya Kwa Mtoto Huyo Ikiwemo Kulegea Kwa Misuli Ya Haja Kubwa Hali Inayomfanya Kushindwa Kuzuia Haja Hiyo Na Kutoa Harufu Mbaya Wakati Wote Kulingana Na Uchunguzi Uliofanywa Na Daktari Wa Hospitali Ya Serikali Ya Mkoa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *