PICHA: Jeneza la Prince Karim Al-Hussaini Aga Khan IV, Kiongozi wa Kiroho wa Waislamu wa Ismailia, likiingizwa kwenye gari la kubebea maiti kutoka Kituo cha Ismailia wakati wa taratibu za kumpumzisha huko Lisbon, Ureno, hii leo Februari 8, 2025.
Kwa mujibu wa Ismaili Imamat, Aga Khan IV, ambaye alifariki siku ya Jumanne mjini Lisbon baada ya takriban miongo saba kama Kiongozi wa kiroho wa Jumuiya ya Kimataifa ya Waislamu wa Ismailia, anatarajia kuzikwa nchini Misri Jumapili ya Februari 9, 2025.






