Rapa 2 Chainz anaendelea vizuri baada ya kukubizwa hopitali baada ya kupata ajali mbaya ya gari iliyotokea leo Jumamosi asubuhi(USA)

Rapa huyo alikuwa akihudhuria Art Basel huko Miami na aliweka video yake akiwa kwenye machela ndani ya gari la kubebea wagonjwa.
Vyanzo vya habari vinasema kwamba rapa huyo amepata majeraha ya shingo na alikuwa ameondoka katika klabu ya Miami ya Booby Trap muda mfupi kabla ya ajali.
