Afungua mlango wa ndege na kutembea juu ya bawa

Jeshi la polisi nchini Mexico linamshikiria abiria mmoja ambaye ni Mwanamume baada ya kufungua mlango wa dharura wa ndege na kutembea juu ya bawa.

Mwanamume huyo alifanya hivyo baada ya ndege hiyo iliyokuwa ikielekea Guatemala City kukwama kwa saa kadhaa kwenye lami bila kiyoyozi wala maji kwa abiria.

Tukio hilo lilitokea Alhamisi iliyopita, baada ya ndege ya Aeromexico kupangwa kusafiri kutoka Mexico City.

Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mexico ulisema hakuna madhara yoyote yaliyotokea, lakini abiria huyo amefikishwa kwa polisi.

Abiria wenzake, hata hivyo, wameandika taarifa ya pamoja, wakisema mtu huyo aliungwa mkono na kila mtu.

Tukio hilo lilitokea Alhamisi iliyopita, baada ya ndege ya Aeromexico kupangwa kusafiri kutoka Mexico City.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *