Jeshi la Polisi Mkoani Tanga limethibitisha kifo cha Mwanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Chief Mang’enya iliyopo wilayani Muheza, Abdallah Msenga aliyefariki baada ya kugongana kichwa na mchezaji wa timu pinzani wakati wakigombea mpira.
Kamanda wa Polisi Mkoa Tanga, Almanus Muchunguzi amesema, tukio hilo limetokea Februari 22, 2026 kwenye uwanja wa shule hiyo, wakati wa mechi ya ligi ya ndani, iliyozikutanisha timu ya kidato cha nne mkondo AB dhidi ya ile ya mkondo CB.

Amesema, Mwanafunzi huyo alikuwa akigombea mpira na mchezaji mwenzake wa timu pinzani, Abdallah Bakari ndipo walipogongana vichwa na kuanguka chini.
“Waligongana na marehemu aligonjwa sehemu ya kushoto, na kukimbizwa katika hospitali teule ya Wilaya ya Muheza ingawa alipoteza maisha wakati akipatiwa matibabu,” alisema Kamanda Muchunguzi.