ADUI WA MWANAMKE SI MWANAMKE – LAMATA LEAH

Muongozaji na mmiliki wa kampuni ya Lamata Village inayojihusisha na kuandika na kutayarisha maudhui na tamthilia mbalimbali kwenye runinga Leah Richard Mwanampoto maarufu kama Lamata Leah amesema adui wa mwanamke si
mwanamke.

Chanuo msimu wa pili umemtafuta na kuzungumza nae kuhusu uthubutu wa
kupambana na watu waliomtangulia katika kuandaa maudhui hayo na ubunifu gani
anaoutumia.

Lamata tumemshuhudia akifanya vitu vizuri ikiwemo tamthilia ya Kapuni na sasa
Juakali ambazo zote zina mafundisho makubwa sana katika Maisha ya kila siku.
Amesema anajivunia sana mafanikio aliyoyapata kutokana na hiki anachokifanya
kitu ambacho hakuwahi kukifikiria katika maisha yake kwa kutoa ajira kwa
Watanzania japo si za muda mrefu lakini zinamfanya mtu kukidhi mahitaji yake ya
kila siku.


“Nina miaka kumi sasa katika tathmilia hii japo mwanzo haikuwa rahisi na hiki kitu
sikusomea ni kipaji kilichomo ndani yangu maana nilianza kuandika hadithi na
zaidi na utotoni nilipenda nikiwa mkubwa niwe polisi lakini tamanio hilo
likatoweka na kujikuta nimejikita kwenye uandishi”


Ameongeza kuwa katika mafanikio yake wanawake wengi wamemshika mkono
akiwemo Jenipha Kyaka, Kajala Masanja, Jackline Wolper na Nisha na kukanusha
wanaosema adui wa mwanamke ni mwanamke.


Akiizungumzia tamthilia ya Jua kali ambayo hivi sasa inafanya vizuri hasa uigizaji
wa Anna na Regina vitu wanavyovifanya katika ndoa zao amesema ni funzo
kubwa sana kwa sababu kila siku katika tamthilia hiyo kuna funzo kubwa sana kwa
mwanamke.


Lamata ametaja changamoto ambazo anakutana nazo katika kazi yake ni uhaba wa
maeneo mazuri ya kufanyia kazi lakini pia kuna wengine wangauswa na tamthilia
na kupelekea kutukanwa na baadhi ya mashabiki na wengine kutoa mawazo yao
ambayo wakati mwingine yanakuwa tofauti na mlolongo ulivyo.


Amebainisha kuwa tathnia hii inawanaume wengi wenye majina na uzoefu
mkubwa lakini alisimamia kile alichokiona ni mwanga wa mafaniko yake licha ya
watu wengi kuinuka kumkatisha tamaa.

Kadhalika akatoa wito kwa wanawake “cha kwanza mwanamke ajivunie kuwa
mwanamke na kuzaliwa mwanamke kwenye hii dunia ni kitu kikubwa sana
nayehisi ni kitu kibaya anakuwa anafanya vibaya cha pili mwanamke anatakiwa
kuwa shupavu ajue natakiwa kufanya nini katika maisha na ahakikishe anatimiza
ndoto zake uwanamke wake tuuone wanaosema mimi ni mwanaume na wewe
useme mimi ni mwanamke ili twende sawa”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *