ADESINA: TANZANIA INATEKELEZA ILICHOPANGA

Rais mstaafu wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), Dkt. Akinwumi Adesina, amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoweka malengo na kuyatekeleza kwa vitendo, jambo lililoifanya kuwa mfano wa maendeleo barani Afrika.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa Bwawa la Umeme la Julius Nyerere, leo Agosti 22, 2026 Dk Adesina, amesema alifurahia kushirikiana na Tanzania katika utumishi wake wa miaka 10 akiwa Rais wa AfDB.

Rais mstaafu wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), Dkt. Akinwumi Adesina.

Amesema juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan zinaonekana wazi kupitia ujenzi wa miundombinu, upanuzi wa fursa za kiuchumi na ukuaji wa sekta ya viwanda.

Kwa mujibu wake, mafanikio ya mradi wa Julius Nyerere hayapimwi kwa megawati pekee, bali kwa mchango wake katika kuimarisha viwanda, kuongeza ajira, kukuza elimu na kuchochea maendeleo ya sekta nyingine.

Dk Adesina, amesisitiza kuwa mradi huo unapaswa kuwa msingi wa utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 na kuongoza mageuzi mapya yatakayobadilisha uchumi wa Tanzania kwa miaka ijayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *