Staa wa muziki Adele ameweka wazi kufunga ndoa na mpenzi wake Rich Paul.
Mwimbaji huyo alitoa siri hiyo katika tamasha la la rafiki yake Alan Carr, lililofanyika nchini Marekani mnamo Novemba 18, 2023.
Adele alivalishwa pete ya uchumba na Paul tangu 2021. Na kwa mara ya kwanza walikutana kwa kwenye sherehe miaka kadhaa iliyopita.
Hii ni ndoa ya pili kwa mrembo huyo ambaye 2019, alipeyana talaka na aliyekuwa mumewe Simon Konecki.