Mwanaume mmoja nchini Nigeria, aliyetambulika kama Adeleke583, amedai kuwa amefanya muamala wa kaisi cha ₦ 500,000 ambao sawa na Tsh/= 1,558,603.38 kwenye akaunti ya David Adeleke, ambaye ni Davido.

Adeleke583 amedai kuwa muamala huo alikusudia kumtumia rafiki yake lakini kwa bahati mbaya amekosea tarakimu kadhaa na kwenda kwa staa huyo hivyo anaomba pesa hiyo arudishiwa.
“Nilikosea kutuma naira #500,000 kwenye akaunti yako ya Benki ya Wema na nambari hii ya akaunti: 0123044967. Hii ilitakiwa kutumwa kwa rafiki yangu ambaye pia anajulikana kwa jina la David Adeleke, Naomba anisaidie hela hiyo irudi.”
