Vanessa Barton Bukuku mwenye umri wa miaka 19, mkazi wa Mtaa wa Kanani Kata ya Makambini katika Mji wa Tunduma mkoani Songwe amekutwa amefariki baada ya kuchinjwa na mwili wake kufichwa kwenye uvungu wa kitanda nyumbani kwao.
Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Songwe Theopista Mallya amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kueleza kuwa uchunguzi bado unaendelea kubaini wahusika wa tukio hilo.
Kamanda Mallya amesema taarifa za awali zinaonyesha kuwa binti huyo alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mtu mmoja ambaye hakumtaja kwa maelezo kuwa wanaendelea na uchunguzi huku akiwataka wananchi wa eneo hilo kutoa taarifa ambazo zitasaidia kuwanasa waliotekeleza unyama huo.