Kwa mujibu wa takwimu za Global Digital Artists Ranking kwa mwezi huu wa nane, zilizotoka Agosti 26 zinaonyesha kuwa staa wa muziki Bongo Diamond Platnumz ameshika nafasi ya 150 Duniani na nafasi ya tisa katika Bara la Afrika kupitia ngoma yake ya Achii…aliyomshirikisha #Koffieolomide.

Ngoma ya Achii imetoka na sasa ina wiki takribani mbili huku video ikiwa imefikisha watazamaji Milioni 5.7 kwenye mitandao wa YouTube.
Mbali na staa huyu kuna Burna boy anashika nafasi ya 4 duniani na Afrika nafasi ya kwanza, ila amewakanyaga wasanii kama DJ Maphorisa, Kabza De Small, Olamide, Fally Ipupa na wengine.
