Na Afarah Suleiman, Babati – Manyara.
Mkuu wa Wilaya Babati, Emmanuela Kaganda amewataka Wananchi wa Wilaya hiyo, kuepuka kujihusisha na vitendo vya kihalifu na badala yake wajitokeza kwenda kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29.
Rai hiyo ameitoa alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwakwe l, akisema hali ya ulinzi na usalama katika wilaya hiyo imeimarika, hivyo ni vyema Wananchi wakajikita katoka zoezi la kupiga kura na kuacha ushabiki wa kwenye mitandao ya kijamii.

Baadhi ya Vijana wakiwemo Maafisa Usafirishaji Wilayani humo, wamesema wamejiandaa kikamilifu kushiriki uchaguzi huo.


