Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Acheni uhuni, dawa za Malaria zinatolewa bure.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amewataka wananchi kote nchini kuhakikisha wanatibiwa bure ugonjwa wa Malaria na wasikubali kulipa fedha yoyote kupata vipimo, matibabu ikiwemo dawa au sindano.

Amesema kumekuwa na uhuni unaendelea katika vituo vya afya huku akisisitiza kuwa matibabu yote ya ugonjwa wa Malaria yanatolewa bure kwakuwa dawa zake zipo katika miradi misonge. Waziri Ummy ameyasema hayo leo Jumatano, Agosti 9, 2023 akiwa Temeke wakati akiendelea na ziara yake ya kutatua changamoto ya ufinyu wa maeneo unaozikabili hospitali na vituo vya afya mkoa wa Dar es Salaam.

“Wataalamu waache uhuni, dawa za Malaria zinapaswa kutolewa bure, bila malipo yoyote hii naisema wazi na wananchi wengi hawatambui hili, kuanzia kipimo cha haraka cha malaria, sindano ya Malaria kali na hata dawa ni za miradi misonge,” amesema Waziri Ummy.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *