Acheni tabia ya kuwadhalilisha viongozi

Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Abdulraham Kinana amekemea tabia ya baadhi ya viongozi wa kisiasa hapa nchini kuwabeza na kuwadhalilisha viongozi watendaji wa serikali katika majukwaa ya kisiasa hali ambayo inapelekea kudhoofisha utendaji kazi wao.

Kinana ameyasema hayo leo Disemba 13 ,2023 wakati akifumgua Ofisi Mpya ya CCM Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita ambapo amesema kufanya hivyo sio vizuri na kuwataka kuzingatia sheria mbalimbali za utumishi na inapotokea watendaji wamekosea wawaelekeze kwa kuzingatia sheria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *