Jambo La Leo

Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Acheni kuwadharau wakuu wa shule

Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt. Charles Msonde amekemea kitendo cha baadhi ya viongozi wa halmashauri nchini kuwanyang’anya wakuu wa shule jukumu la kusimamia miradi ya ujenzi wa miundombinu ya shule kwa kudhani kuwa hawana uwezo wa kusimamia miradi hiyo.

Dkt. Msonde amekemea tabia hiyo wakati wa kikao kazi na viongozi wa mkoa na halmashauri kilicholenga kufanya tathmini na majumuisho ya ziara yake ya kukagua ujenzi wa miundombinu ya elimu mkoani Rukwa.

Dkt. Msonde amesema uzoefu unaonesha kuwa, popote pale ambapo wakuu wa shule wamenyang’anywa jukumu lao la kusimamia utekelezaji wa miradi, miradi hiyo haijakamilika kwa wakati kama ilivyokusudiwa na Serikali.

Dkt. Msonde ameanisha kuwa, Serikali ilipoamua kupeleka shuleni fedha za ujenzi wa miundombinu haikukosea kwani iliwapa hadhi wakuu wa shule kuwa maafisa masuuli, hivyo Wakuu wa Wilaya na Makatibu Tawala wa Wilaya wanaowajibu wa kuwalinda walimu wakuu wasinyang’anwe majukumu yao ili kulinda jukumu walilopewa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *