Jambo La Leo

Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

“Acheni kuongea ongea, Wakikuona wa maana watakuita”

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi CCM, Paul Makonda amesema sio utaratibu kwa Wastaafu kila siku kuongea ongea huku akiwashauri Wastaafu wakishapumzika watulie na walee Familia zao na kwamba kama watahitajika kwa ajili ya kazi wataitwa.

Akiongea Jijini Dodoma leo Makonda amesema Kuna tofauti kubwa kati ya waliokwenda Mjini kwa kuungaunga na wale waliowakuta Mjini, kwani waliokwenda mjini kwa kuungaunga wamepigana vita na mapori mengi ,na kuwataka waliopo ndani ya CCM na nje ya CCM wampee nafasi Rais afanye kazi yake.

“Ukishaitwa Mstaafu tulia lea Familia yako wakikuona wa maana watakuita kama walivyomuita Makonda, huwezi kuwa Mstaafu halafu kutwaa, aah, aah, na Wastaafu Nchi hii wanaheshimika sana na Mimi nimejifunza kutoka kwao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *