Endapo kwenye ulimwengu wa mahusiano kila mmoja angejitambua, akafuata misingi sahihi ya uhusiano, basi kusingekuwa na ugomvi, lakini kutokana na ugumu wa mioyo yetu, tunaifanya dunia kuwa uwanja wa mapambano. Watu wanagombana kila kukicha, wanapi
Ukichunguza kwa ukaribu chanzo kikuu cha matatizo haya huwa ni usaliti na Tamaa ambazo zinawatesa watu, wanashindwa Maisha yao na wapenzi wao na unakuta watu wengine hata siyo tamaa ya kitu au vitu, bali ni tabia tu.
Ila lazima tutambue hakuna binadamu aliyekamilika. Kila mtu ana upungufu wake, hivyo unaweza kujiona upo sahihi kumbe wewe ndiye tatizo. Ni vizuri kuruhusu akili yako ijifunze kutoka kwa wanaokuzunguka.
Unapokutana na makwazo fulani kwenye uhusiano yako, kikubwa wewe ‘jipe muda zaidi kwa kutafakari’. Usiruhusu kufanya uamuzi magumu kipindi unapokuwa na hasiara, kwani hasira hasara na ndio maana unasikia ameua, amejinyonga au wameachana hizi ni hasira, wewe jenga desturi ya kupuuza fanya jambo lingine ambalo litakutoa kwenye mawazo hayo.
Hakuna cha maana mnachokuwa mmekipata zaidi ya kuishia kwenye matatizo makubwa. Ukitafakari kwa kina baada ya tatizo kutokea, unaona kumbe ungejizuia wala msingefikia hatua mliyofikia.
Kaa mbali na mpenzi wako unapokuwa na hasira. Ondoka, nenda mahali pengine ambako utakutana na mazingira na watu tofauti. Utachangamka, ukirudi kwa mtu wako huwezi kuwa yule wa kwanza