Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara linamshikilia kijana mmoja mwenye umri wa miaka 14 mkazi wa kijiji cha Mnete Kitongoji cha Chiano Kata ya Nalingu iliyopo halmashauri ya Wilaya ya Mtwara kwa tuhuma za kubaka na kunajisi watoto wawili wanaodaiwa kuwa ni wa familia moja.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara, Nicodemus Katembo amesema mtuhumiwa anayedaiwa kufanya matukio hayo ni kaka wa Watoto hao na alitekeleza kwa nyakati tofauti.
Amesema alimbaka mtoto wa kike (7) na kumsababishia maumivu makali katika sehemu zake za siri na kisha kumnajisi mtoto wa kiume (5) na kumsababishia maumivu katika sehemu yake ya haja kubwa.
Kamanda Katembo ameongeza kuwa kiini cha tukio hilo ni tamaa za kimwili hivyo ametoa rai kwa wananchi mkoani humo, kuendelea kushirikiana na jeshi hilo kupinga unyanyasaji na ukatili wa kijinsia pamoja na maadili yanayokinzana na sheria za nchi.