WAKULIMA NCHINI WASHAURIWA KUCHUKUA MKOPO.

Wakulima nchini wameshauriwa kuchukua mikopo kwa malengo ili kuondokana na mkianganyiko ya kudaiwa madeni inayotokea pale wanapokuwa wameshindwa kulipa marejesho.

Usahuri huo umetolewa Machi 20, 2025 hapa Jijini Dodoma na Mkulima wa zao la zabibu kutoka Mpunguzi Justin Mwasa wakati akizungumza na Jambo FM kwa njia ya simu hii ikiwa ni kufuatia taarifa iliyotolewa na Benki ya Maendeleo TIB kuwa imewekeza takribani shilingi bilioni 162 katika Sekta ya Kilimo ambapo inalenga kuongeza tija na kuboresha maisha ya wakulima nchini.

“Nawashauri wakulima wenzangu kuwa unapoenda kuchukua mkopo tuchukue mkopo kwa malengo, sio unachukua tu huna malengo mwisho wa siku unaanza kudaiwa deni ambalo kiasi kwamba ukitaka kulipa unaona unalipa hasara,”amesema.

Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIB, Lilian Mbassy, amesema kuwa hatua hiyo imefanikisha miradi ya kilimo katika mikoa 23 na wilaya 76 ambapo asilimia kubwa ya fedha hizo inatokana na mikopo ya bei nafuu.

“Uwekezaji huu umefanikisha miradi ya kilimo katika mikoa 23 na wilaya 76. Asilimia kubwa ya fedha hizi inatokana na mikopo ya bei nafuu kupitia dirisha la kilimo tunalosimamia kwa niaba ya Serikali chini ya Wizara ya Fedha,” amesema Mbassy.

Ameongeza kuwa uwekezaji huo umesaidia kuzalisha ajira zaidi ya 15,000 na kunufaisha vyama vya ushirika vya akiba na mikopo (SACCOS) takribani 78 nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *