Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Wakandarasi waonywa, Tanesco Shinyanga ikidai bilioni 3.7 

Naibu waziri Mkuu na waziri wa Nishati Dkt. Dotto Mashaka Biteko amewataka wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme nchini kuhakikisha wanatekeleza miradi kwa wakati na kuhakikisha wanafanya kazi walizopewa na kueleza kwamba hawatomuangalia usoni yeyote atakayekwamisha miradi katika kipindi ambacho Rais Dkt Samia Suluhu Hassan anahangaika kutafuta fedha za utekelezaji wa miradi.

Ameyasema hayo Machi 14,2024 baada ya kuweka jiwe la msingi la Mradi wa ujenzi wa Umeme jua wa megawati 150 unaotekelezwa katika kijiji cha Ngunga kata ya Talaga wilayani Kishapu mkoani Shinyanga na kubainisha vijiji ambavyo vimefikiwa na nishati ya umeme kwa mkoa wa Shinyanga pamoja na kuwataka wale wote wanaodaiwa na TANESCO mkoa wa Shinyanga,deni lililofika kiasi cha shilingi bilioni 3.7 kulipa haraka fedha hizo.

Awali akisoma taarifa ya Mradi huo,Kaimu Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) Mhandisi Costa Lubagumya ameeleza kwamba fedha iliyotengwa kwaajili ya utekelezaji wa mradi huo ni kwamba awamu ya kwanza ya utekelezaji wamradi huo itagharimu kiasi cha shilingi bilionoi 118.677 na fedha iliyotekwa kwa utekelezaji wa awamu ya pili ya mradi huo ni kiasi cha shilingi bilioni 204.419 ambapo jumla ya fedha zilizotengwa kwa awamu zote ni kiasi cha shilingi bilioni 323.096.

Kati ya hizo shilingi bilioni 320.255 za kitanzania ni mkopo kutoka Shirika la Maendeleo la Ufaransa(AFD) na shilingi bilioni 2.841 ni fedha kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilizotumika kama malipo ya fidia kwa wananchi waliotoa maeneo yao kupisha mradi.

Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa(AFD) Bi.Celine Robert amesema mafanikio ya utekelezaji wa mradi huo ambao ni sehemu ya makabiliano ya athari za mabadiliko ya tabianchi yametokana na ushirikiano wa muda mrefu kati ya Tanzania na Ufaransa na umelenga kuzalisha umeme jua kwa lengo la kuwawezesha wananchi kupata umeme wa uhakika.

Daudi Mwanabolingo,Mussa Manoni na Salome Amos Sangwa ni miongoni mwa wananchi waliohudhuria katika hafla hiyo wameishukuru serikali kwa kutekeleza mradi huo na kueleza kwamba utawasaidia kuwakwamua kiuchumi kwa ongezeko la nishati pamoja na uapatikanaji wa fursa za ajira wakati wa utekelezwaji wake.

Mradi wa huu umeme jua wa megawati 150 unaotekelezwa wilayani Kishapu unaelezwa kuwa ni mradi mkubwa na wa kihistoria wenye upekee wake kwa ukubwa ambao ni wa kwanza kwa nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara na katika awamu ya kwanza uatekelezwa na kampuni ya Sinohydro Corporation kutoka China ambapo mkataba wa ujenzi ulianza kutekelezwa Desemba 8,2023 ukitarajiwa kukamilika mwezi Januari mwaka 2025.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *