Erimina Clement Marandu (40) maarufu kwa jina la Pendo ambaye ni Ofisa Kilimo Wilaya ya Moshi, amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Moshi akikabiliwa na kosa la kumjeruhi mfanyakazi wa ndani Meresiana Nestory (16) kwa kumpiga na mti wa fagio na mateke na kumsababishia majeraha katika sehemu mbalimbali za mwili wake.
Mshitakiwa huyo ambaye ni mwenyeji wa Rombo amefikishwa mahakamani hapo leo Jumatano, Machi 13, 2024 mbele ya Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama hiyo, Ruth Mkisi.
Katika kesi hiyo ya jinai namba 38/2024 inadaiwa kuwa, mshitakiwa huyo kwa nyakati tofauti kati ya Januari na Februari mwaka huu, alimjeruhi msaidizi huyo wa kazi za ndani kwa kumpiga sehemu mbalimbali za mwili wake kwa kutumia fimbo, fagio na mateke.