Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Dawa za kulevya zilinipoteza – Mr. Blue

Staa wa muziki Bongo flava, Mr. Blue amekiri kuwa kuna kipindi alipotea kwenye müziki kutokana na kufuata starehe na marafiki wabaya ambapo ikapeleka kuingia kwenye madawa ya kulevya.


Akifanya mahojiano na BBC Swahili, Mr Blue amefunguka kuwa familia ndio chanzo kikubwa yeye kurudi kwenye ramani kwani aligundua kuwa ameshaingia kwenye majukumu ya kifamilia.

“Mimi wakati naanza muziki nilikuwa mtoto na sikuwa na rafiki lakini watu walikuja wakijifanya wananijua wamesoma na mimi kwahiyo ule ushkaji mtu akichoma na mimi nachoma mara pombe nikawa siendi studio, Mimi nimeharibiwa na watu waliokuja baada ya mimi kuwa Staa,” amesema Mr Blue.


Akasisitiza “Mimi mke wangu namshukuru sana kwani yeye ndio amechangia kwa kiasi kikubwa mimi kubadilika, Alikuwa ananiambia taratibu vitu vya kufanya na badae aliposhika ujauzito ndio nikagundua naenda kuwa na familia.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *