Cristiano Ronaldo ndio anavuta mkwanja mrefu Instagram

Utafiti  uliofanywa hivi karibuni  na mtandao wa Influencer MarketingHub, umeweka orodha ya watu 10 mashuhuri Duniani wanoongoza kulipwa pesa nyingi kwa kuposti kwenye mtandao wa Kijamii wa Instagram.



Cristiano Ronaldo ndio mtu maarufu  anayeongoza kulipwa pesa nyingi kwa kuposti tangazo kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram akiwa na wafuasi milioni 622, ambapo anakadiriwa kulipwa wastani wa $3,234,000 (sawa na TZS Bilioni 8.246) kwa post moja tu.



Orodha ya watu hao.

1. Christiano Ronaldo – TZS Bil. 8.2
2. Lionel Messi – TZS Bil. 6.6
3. Selena Gomez – TZS Bil. 6.5
4. Kylie Jenner – TZS Bil. 6.1
5. Dwayne Johnson – TZS Bil. 5.9

6. Ariana Grande – TZS Bil. 5.8
7. Kim Kardashian – TZS Bil. 5.5
8. Beyonce Knowles – TZS Bil. 4.8
9. Khloe Kardashian – TZS Bil. 4.7
10. Justin Bieber – TZS Bil. 4.5

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *