Miaka 8-9 iliyopita staa wa muziki Diamond Platnumz aliimba na Iyanya ngoma mbili ambapo walitumia lugha ya kiswahili na this time Rayvanny ameingia studio na msanii huyo na wanarekodi kazi.
Rayvanny ambaye kwa sasa yupo nchini Uingereza akifanya kazi zake za muziki, ameweka picha kadhaa kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa studio na msanii huyo pamoja na watu wengine wakiwa wanarekodi kazi.