Ni takribani siku 28 sasa tangu tuanze mwaka 2024, Hivi unajua wa taalamu wa rangi, ambao wanajulikana kama kampuni Pantone wameitaja rangi ya peach fuzz ndiyo rangi ya mwaka 2024.
Rangi hii inatajwa hufariji mtu katika nyakati zote na Peach kimsingi ni rangi kama ya chungwa iliyokolea sana, kwa hiyo ina hisia ya joto, nishati, na urafiki.
Kwa mujibu wa Pantone, rangi ya peach fuzz ni rangi inayomaanisha huruma na wema wa kutoka moyoni.
Vile vile rangi hii ni maarufu katika tamaduni za magharibi kama rangi ya upole, matumaini baada ya vita na ngozi za watu wa euro-centric,na katika utamaduni wa Kichina, rangi ya peach inawakilisha bahati nzuri na maisha marefu.