
Meneja wa msanii, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Said Fella ‘Mkubwa Fella’ amemmwagia sifa rapa mkongwe, Juma Kassim ‘Sir Nature’ akidai ni mwanamuziki mzuri na bado ana nafasi kubwa ya kuendelea kubamba.
Fella ambaye awali alikuwa meneja wa msanii huyo kabla ya kuhitilafiana takribani miaka 15 iliyopita, ameeleza kuwa ni mambo machache anahitaji kuyaweka sawa ili kuendelea kuonesha ubora wake.
Alisema hata wakati wanaingia kwenye mgogoro alifahamu wanachoshindania kuhusu maslahi hakikuwa na uhalisia kama kinavyoelezwa japokuwa alifahamu Nature ni msanii mkali mno.