Klabu ya soka ya Kahama United FC Kahama United FC siku ya leo imechinja ng’ombe mkubwa kusherehekea ubingwa wa ligi ya taifa, wilaya ya Kahama iliyodhaminiwa na Wakili Sweetbert Nkuba Sr, baada ya kuifunga KMC katika mchezo wa fainali.
Sherehe hizo zilizoanza mapema asubuhi kwa watu mbalimbali kunywa supu, kilele chake kitafanyika kwenye Bwalo la Magereza Kahama, ikiambatana na shughuli kadhaa.
Kama Utoaji wa zawadi (Fedha) kwa wachezaji wa Kahama United ambao wataambatana na wazazi wao.