Usawa wa kijinsia eneo la uchumi kutiliwa mkazo

Waratibu wa Programu ya Jukwaa la kizazi chenye usawa wametakiwa kutambua masuala yaliyowekewa Ahadi hususani upande wa kiuchumi ambapo Tanzania ni kinara wa eneo hilo kwenye Jukwaa la Kizazi chenye Usawa.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima ametoa maelekezo hayo Januari 15, 2024 wakati akifungua mafunzo ya Programu hiyo kwa waratibu wa ngazi za mikoa na Halmashauri yanayofanyika kwa siku mbili mkoani Mwanza na kukamilisha mafunzo kwa mikoa yote 26 na halmashauri 184 nchini.

Waziri Dkt. Gwajima amewaagiza waratibu hao kuratibu Afua zinazotekelezwa na sekta zao na kuzitolea taarifa kwa wakati pamoja na kutambua wadau waliopo na afua wanazotekeleza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *