Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Mwijaku amshukuru Diamond Platnumz

Mwijaku amshukuru Diamond Platnumz, Mama Diamond na kutia neno kuhusu Zuchu baada ya kujenga nyumba yake ya kisasa

“UKWELI-Siwezi kupinga ukweli ..! Safari yangu ya kwanza QATAR ( WorldCup ) na malipo yake ndio yalio nifanya ninunue eneo na kuanza safari yangu ya kujenga KASRI langu ( Ndoto yangu ) Ukweli usemwe , Ulinipa rizki kupitia kampuni yako, nami nikaitumia vizuri , sitakiii kua mchoyo ya kushukuru

Nakumbuka tulipo kua Qatar ulinambia kua “pambana wakati wako huu DC ” nami nikaichukua hiyo kauli .Tarehe 5/01/2024 Nimekamilisha ndoto yangu . Kupitia Kampuni yako ilinipa mkataba zaidi ya miaka miwili na malipo ya kila mwezi na nikatumia kama sehemu ya uwekezaji kwangu .Nasema Asante MWAMBINO Diamond Platnumz sitaki kuja kusubiria ukifa au nikifa ndio yasemwe haya , Ulinifaa wakati wa shida na wakati wa mahitaji Muhimu

Asante kwa Don Fumbwe(Mfanyakazi wa Diamond) Nakumbuka mzigo ulionipa magomeni usiku wa saa mbili baada ya kupokea simu toka kwa mwambino ndio ulizaa uwekezaji huuuu . Asante kwako kwa kua hukunizunguusha kunikabidhi haki yangu

Nimshukuru pia mama mzazi wa MWAMBINO Mama Dangote , ulinipa ushirikiano mkubwa pale QATAR na kunambia fanya kazi uisaidie familia yako na niache CHUKI binafsii . Nika kwambia simchukii MWAMBINO but ni kuchangamsha mitandao yetu Asante kwa kunielewa mama yangu .Haya Mengine ya mtandaoni ni sehemu zetu za kunogesha game na kuhakikisha tunapambana kukuza burudani

Mwenyezi Mungu aendelee kuwapa fikra za kuwasaidia wengine kwa kuwapa kazi na kuwapa usia wa kutumia vizuri vipato wanavyo vipata . Asante kwa hili MWAMBINOOOMungu akubariki wewe na kizazi chako . Sema na mimi nakushaurii OA mkubwa wakati wako huu Muoe ZUCHU Zuchu ana UPEPOO WAKO 🙏🏾 .”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *