Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Uzalishaji wa dawa nchini utasaidia upatikanaji wa dawa ma gharama nafuu

Waziri wa afya Ummy Mwalimu ametoa rai kwa Wadau wa Maendeleo kuunga mkono jitihada za Serikali kwa kuwekeza kwenye Sekta ya Afya nchini huku wakiiga mfano wa Kampuni ya uzalishaji wa Dawa cha Cure Afya ambayo iko mbioni kuanza uzalishaji wa dawa hapa hapa nchini.

Waziri Ummy ameyasema hayo leo Disemba 20, 2023 alipo tembelea Kiwanda kipya cha utengenezaji Dawa cha Cure Afya ambacho kipo Wilaya ya Kigamboni Jiijini Dar Es Salaam kwa ajili ya kuona utayari wa Kiwanda hicho kutengeneza Dawa kwa ajili ya soko la ndani ya nchi pamoja na nchi jirani.

“Dawa zinazozalishwa zitarahisisha upatikanaji wake kwa wakati, tofauti na tukiagiza dawa nje ya nchi zinachukua miezi 6 hadi 9 kuweza kufika hivyo inachukua muda mrefu mpaka kufika nchini”. Amesema Waziri Ummy.

Amesema serikali imejizatiti kukuza uzalishaji wa dawa wa ndani ili kupunguza gharama ya uagizaji kwani Tanzania ni miongoni mwa nchi nne za Afrika ambazo zinatambulika kwa umahiri kupitia Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba TMDA na Shirika la Afya Duniani WHO.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *