Mabingwa watetezi Manchester City watacheza dhidi ya Copenhagen hatua ya 16 bora ya ligi ya mabingwa, wakati Arsenal wakiiva Porto.
Copenhagen, waliomaliza juu ya Manchester United katika kundi lao, wanafika hatua hii ya mtoano kwa mara ya kwanza tangu 2011.
Mechi za mkondo wa kwanza zitachezwa kati ya Februari 13-14 au 20-21 na za mkondo wa pili zitachezwa kati ya Machi 5-6 au 12-13.
DROO KAMILI
Porto v Arsenal
Napoli v Barcelona
Paris St-Germain v Real Sociedad
Inter Milan v Atletico Madrid
PSV Eindhoven v Borussia Dortmund
Lazio v Bayern Munich
Copenhagen v Manchester City
RB Leipzig v Real Madrid