Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Mgeni aua Mama na Mtoto na kuondoka na vichwa vyao

Watu wawili Mama na mtoto wake wakazi wa Kijiji cha Mavimba Wilaya ya Ulanga, Mkoani morogoro wamefariki baada ya kuchinjwa na kutenganishwa vichwa na viwiliwili, na muuaji kuondoka na vichwa vyao.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kijiji cha Mavimba, Salehe Ndoki amesema kuwa mauaji hayo yametokea usiku wa kuamkia novemba 24, 2023.

Uongozi wa kijiji hicho umekemea vikali tukio hilo na kuwataka wanakijiji kufuata taratibu za kupokea wageni kwani Kinachoelezwa ni familia hiyo haikufuata utaratibu wa kuishi na kijana ambaye kwa sasa ametokomea kusikojulikana.

Jitihada za kumtafuta kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro alex Mkama zinaendelea kwa ajili ya kupata undani wa taarifa hii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *