Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

EAC kuongoza vita dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa

Rais wa Kenya, William Ruto amesema ni lazima hatua za kiubunifu na endelevu zibuniwe ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa, Hatua ambazo rais Ruto amesema zitachukuliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati ikielekea Dubai kwa mkutano kuhusu mazingira wa COP28 baadaye mwezi huu.

Akizungumza katika kikao cha wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa na usalama wa chakula jijini Arusha, Rais Ruto amemsema Afrika itatumia na kuonyesha uwezo wake katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Miongoni mwa viongozi wa nchi za EAC wanaohudhuria kikao hicho ni pamoja na Rais Samia Suluhu Hassan (Tanzania), Evariste Ndayishimiye (Burundi) na Salva Kiir (Sudan Kusini).

Aidha Rais Ruto ameeleza kuwa Afrika itatoa wito wa kusainiwa kwa mkataba mpya wa ufadhili ambao utarekebisha mfumo wa sasa wa kifedha wa kimataifa, ambao hauendani na hali ya sasa ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *