Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Upungufu wa umeme wazidi kupungua

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema kuwa hali ya upatikanaji wa umeme nchini kwa kipindi kati ya mwezi Septemba mwishoni hadi kufikia sasa imeendelea kuimarika kutoka upungufu wa megawati 410 hadi kufikia 213 kwasasa.

Hayo yamebainishwa leo Novemba 24 2023 Jijini Dodoma na Mtendaji Mkuu wa TANESCO Eng. Gissima Nyamo-Hanga wakati akitoa taarifa kuhusiana na hali ya upatikanaji wa huduma hiyo nchini.

Eng. Nyamo-Hanga amesema kuwa takribani zaidi ya megawati 197 zimeongezeka katika mfumo wa wa Gridi ya taifa ndani ya kipindi hicho kutokana na juhudi mbalimbali za matengenezo ya mitambo, kuongezeka kwa upatikanaji wa Gesi asilia kutoka TPDC sambamba na upatikanaji wa mvua katika ukanda wa vituo vya kuzalisha umeme na nyumba ya Mungu, Hale na Pangani.

Amesema Shirika litaendelea kuchua hatua mbalimbali ili kukabiliana na upungufu huo wa umeme kwa kuendelea kufanyia matengenezo mitambo yake pamoja na kusimamia kwa umakini zoezi la mgao wa umeme linaloendelea hadi sasa ili kupunguza makali ya mgao. Aidha ameongeza kuwa hali ya upatikanaji wa umeme itaendelea kuimarika katika miezi ya usoni kutokana na kukamilisha matengenezo ya mitambo iliyokuwa na hitilafu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *