Mkoa wako upo nafasi ya ngapi kwa matumizi ya vyoo?

Mikoa inayoongoza kwa kuwa na vyoo bora ni Dar es Salaam (98.5), Ruvuma (92.1) na Njombe (87.6) na mikoa yenye idadi ndogo ya vyoo bora ni Tabora (40.5%), Katavi (52.5%) na Manyara (53.9%). Mikoa anbayo haina vyoo bora ni Katavi (24.3%), Simiyu (24.3%) na Manyara (22.3%).

Kwa mujibu wa Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Dunia ya 2030 “Sustainable Development Goals – SDG 2030”, lengo la 6.2, Nchi zote Wanachama wa Umoja wa Mataifa zinatakiwa kuhakikisha watu wote wanatumia vyoo bora na salama yaani “Safely Managed Sanitation” ifikapo mwaka 2030.

Taarifa ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ya mwaka 2022 inaonesha kuwa asilimia 57 pekee sawa na watu Bilioni 4.6 Duniani wanatumia vyoo bora na salama.

Ripoti ya Tafiti ya Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria ya Mwaka 2022 (Demographic and Health Survey and Malaria Indicator Survey) imeonesha kuna ongezeko kubwa la watu wanao tumia vyoo bora kutoka asilimia 21 mwaka 2016 hadi asilimia 74.8 mwaka 2022. Takwimu hizi ni hatua chanya katika kufikia lengo la 6.2 la SDG ifikapo mwaka 2030.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *