Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Tanzania ina akiba ya dola bil. 5.1 zinatosha kwa miezi minne

Gavana wa benki kuu ya Tanzania Emmanuel Tutuba amesema hadi sasa Tanzania ina akiba ya fedha za kigeni zaidi ya dola za kimarekani bilion 5.1, fedha ambazo zinakidhi uingizwaji wa bidhaa na huduma nyingine hapa nchini kwa takribani miezi minne.

Tutuba ameyasema hayo wakati akiwa katika mahafali ya pili ya chuo cha benki kuu Jijini Mwanza ambapo amesema bado kiwango cha upungufu wa fedha za kigeni hapa nchini ni mdogo ukilinganisha na upungufu uliopo nchi nyingine kwani hadi sasa fedha zilizopo zinaweza kutumika kwa miezi 4.9 na amewataka wananchi waendelee kufanya shughuli za kiuchumi ili ziweze kuongeza upatikanaji wa fedha za kigeni hapa nchini.

Katika hatua nyingine Tutuba amesema Benki Kuu inaendelea kuboresha mfumo wa upatikanaji wa wataalamu wenye uadilifu katika sekta ya hiyo ya fedha ili kuhakikisha wananchi wanakua na imani na benki hiyo pale wanapokwenda kuweka fedha zao.

Kwa upande wake mkuu wa chuo cha benki kuu ya Tanzania Dkt. Nicas Yabu amesema mpaka sasa chuo cha Benki Kuu Tanzania kimeanza kuandaa mtaala wa cheti cha umahiri wa ithabati kwa waelimishaji wa fedha ili kuweza kuwatambua na kuwarasimisha watu wanaohusika na maswala ya fedha ili watu hao wasiendeshe shughuli zao kiholela.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *