Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Wajadili kuhusu uagizaji madini ya chumvi nje ya nchi

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde pamoja na waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji, Watendaji na Wataalam wa Wizara hizo mbili wamekutana na kufanya kikao cha pamoja kuhusu mustakabali wa Uagizwaji wa madini ya chumvi kutoka nje ya nchi.

Awali, kikao hicho kilipokea taarifa ya takwimu za chumvi zilizoko maghalani hivi sasa kwa ajili ya kutathmini hali ya uzalishaji wa chumvi nchini sambamba na kulisha viwanda vya usindikaji bidhaa hiyo.

Kikao hicho pia kilipokea taarifa ya ununuzi wa madini ya chumvi uliofanywa na kiwanda cha Neelkanth Salt Limited na kutaka kufahamu ikiwa chumvi ghafi ilifuatwa mashambani au wauzaji walipeleka kiwandani kwa ajili ya usindikaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *