Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Magonjwa yasioambukiza imekuwa changamoto Barani Afrika

Imeelezwa kuwa magonjwa yasioambukiza imekuwa changamoto Barani Afrika ikiwemo shinikizo la damu (presha) na Kisukari.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi Magonjwa yasioambukiza Wizara ya Afya Dkt. Omary Ubuguyu katika uzinduzi wa madhimisho ya wiki ya magonjwa yasioambukiza iliyoandaliwa na Wizara ya Afya, Ofisi ya (TAMISEMI) uongozi wa Mkoa wa Dar es salaam pamoja na wadau wa huduma za magonjwa yasioambukiza.

Dkt. Omary amesema utafiti unaeleza katika watu 100 watu watano wana ugonjwa wa Kisukari na Shinikizo la damu hivyo amewataka wananchi kushiriki mazoezi na kuweka mpangilio wa vyakula kiafya.

Aidha Dkt.Omary amesema utafiti unaeleza kuwa umri wa kuishi kwa wanawake ni miaka 69 na wanaume umepungua kwa sasa wanaishi miaka 62 kwa ajili ya changamoto mbalimbali ikiwemo mabadiliko ya tabianchi,mazingira na mabadiliko katika maendeleo.

Mganga Mkuu Mkoa Dar es Salaam Rashid Mfaume amesema siku ya Magonjwa yasioambukiza Kitaifa mwaka huu yatafanyika Mkoa Dar es Salaam Novemba 14 mpaka 18 ambapo magonjwa mbalimbali yatapimwa viwanja vya Mnazi Mmoja na madaktari bingwa watakuwepo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *