Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Watoto zaidi ya laki mbili ni wahanga wa mitandao ya kijamii

Imeelezwa kuwa teknolojia na matumizi ya mtandao hususani matumizi ya simu janja imekuwa kichocheo kikubwa cha mmomonyoko wa maadili kwa watoto na kuiga mila na desturi za mataifa ya magharibi huku wito ukitolewa kwa mamlaka ya mawasiliano tanzania kubuni mikakati na mbinu zitakazowalinda watoto na maudhui hatarishi wanapotumia mitandao na kuhakikisha wapo salama.

Jambo Fm imezungumza na baadhi ya wakazi katika manispaa ya shinyanga kuhusiana na tukio hilo baada ya kuibuka kwa sehemu za kutumia mitandao (intaneti café) na wamiliki kutoweka zuio la watoto kufika katika maeneo hayo huku baadhi ya wazazi wakijitahidi kununua simu janja ambazo zinasaidia kutekeleza shughuli kadhaa mtandaoni hali iliyopelekea watoto kutambulishwa katika matumizi ya mtandao hasa kwa wale wanaoachwa na wazazi kutumia simu hizo.

Tahadhari imeelekezwa pia kwa kada ya waliohitimu darasa la saba mwaka huu na mkuu wa chuo kikuu huria tawi la Shinyanga Agatha Mgogo ,kwa wazazi kuwa makini na watoto hao ambao watakaa nyumbani muda murefu kusubiri matokeo huku akihimiza wazazi hao kutowapa simu janja ili wawe salama na maudhui mabaya ya mtandaoni ili kutimiza ndoto zao.

Ripoti ya usalama wa watoto mtandaoni inaonyesha takribani watoto 200,000 tanzania ni wahanga wa kurubuniwa au kudhalililishwa kingono mtandaoni huku 3% kati ya watoto hao walijirekodi na kurusha maudhui ya utupu mtandaoni wakati 5% kati ya watoto hao wameonyesha tabia hatarishi ikiwemo kukutana na watu wasiowafahamu na 2% kati ya hao walitishiwa mtandaoni wakilazimishwa kujihusisha na vitendo vya kingono.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *