Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

TARURA Shinyanga yajipanga na mvua za El-Nino

Meneja wa wakala wa barabara vijijini na mijini TARURA mkoa wa Shinyanga Mhandisi Oscar Gilbert amesema katika kukabiliana na changamoto za barabara mbovu kuelekea kipindi cha mvua za e-El-nino wameandaa mikakati mbalimbali ya kuhakikisha barabaraza hizo zinafanyiwa matengenezo ikiwemo kuzibua madaraja na mitaro mikubwa katika baadhi ya kata mkoani Shinyamga.

Mhandisi Gilbert amesema hayo leo wakati akizungumza na Jambo Fm na kuwataka wananchi kuwa na uvumilivu kwa kipindi hiki kufuatia changamoto za barabara wanazokumbana nazo katika maeneo yao.

Aidha amewasihi wananchi kuendelea kutunza miundombinu kupitia shughuli mbalimbali za kibinadamu ikiwemo kilimo na ufugaji vilevile kuondokana na tabia ya kutupa taka katika mifereji na mitalo ya barabara.

Pamoja na hayo ameomba ushirikiano wa wananchi katika utunzaji wa miundombinu kwa kujitolea kufanya shughuli za utunzaji wa miundombinu hiyo kama vile kuzibua mitalo na mifereji iliyoziba katika maeneo yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *