Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Jela Maisha kwa kumnajisi mtoto wa miaka 8

Mahakama ya Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, imemuhukumu mkazi wa Kijiji Cha Chapulwa, Kata ya Mwendakulima, Kaliyango Maganga (55) kifungo cha maisha jela kwa kosa la kumnajisi mtoto mwenye umri wa miaka nane 8) anayesoma darasa la kwanza.

Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Christina Chovenye ametoa hukumu baada ya kuridhika kuwa mshitakiwa alifanya kosa hilo kwa mtoto huyo mara kwa mara,ambapo alifikishwa mahakamani Julai 30, 2023.

Hakimu Chovenye alisema mshtakiwa alikuwa na kazi ya umwagiliaji bustani ya maua nyumba ya jirani na mtoto huyo, ambapo alikuwa akimvizia wakati akienda shule walezi wake wakimuacha peke yake na kwenda kwenye shughuli za uchimbaji madini katika Mgodi wa Mwime.

Hakimu Chovenye amesema mtoto mwenyewe alisikilizwa na kutoa maelezo ya kunajisiwa na mtuhumiwa mara kwa mara na vipimo vya daktari vimethibitidha, hivyo mahakama haikuwa na shaka lolote juu ya utoaji wa hukumu hiyo.

Pia ushahidi wa walimu ambao waligundua mtotp huyo kunajisiwa na kueleza kuwa kila siku alikuwa akichelewa shule na akifika anakuwa amechoka na mwenye maumivu makali.

Mshtakiwa akijitetea aliomba apunguziwe adhabu hiyo kwa madai ni mzee na anategemewa na familia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *