TAARIFA MPYA YA UTEUZI WA RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali ambapo Prof. Tumaini Nagu ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia masuala ya afya.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka pia Dkt. Blandina Kilama ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango
anayeshughulikia biashara na ubunifu, akichukua nafasi ya Dkt. Lorah Madete ambaye uteuzi wake umetenguliwa na atapangiwa majukumu mengine.

Balozi George Kahema Madafa, yeye ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Puma Energy Tanzania, akichukua nafasi ya Dkt. Majige Budeba
ambaye amemaliza muda wake.

Aidha, Jacob Jail Kibona naye ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) kwa kipindi cha pili, huku Meja Jenerali Mstaafu John Julius Mbungo akiteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi ya Kampuni ya Meli Tanzania (TASHICO) kwa kipindi cha pili.

Mussa Hamza Mandia ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kwa kipindi cha pili, ambapo uapisho wa Naibu Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mtendaji utafanyika baadaye.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *