
Mbunge wa Jimbo la Kisesa lililopo Mkoani Simiyu, Mhe. Luhaga Mpina ameliomba bunge kuazimia kuifuta wizara ya Viwanda na Biashara kwa madai ya kuwepo kwa bidhaa feki nchini zinazohatarisha Afya za watanzania kinyume na kazi za wizara hiyo.
Mhe. Mpina ameyasema hayo wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa mwaka wa fedha 2025/26.
“Leo kuna viwanda bubu vinavyotengeneza vinywaji wananchi wetu wanakunywa vinywaji vingapi kutoka kwenye viwanda hivyo wizara inayohusika iko wapi na leo hii kupitia wizara hii waliondoa kigezo cha COC kuwa kigezo cha kuingiza bidhaa nchini leo bidhaa feki zimejaa kila kona kila mtu anakiri leo hii wananchi wanapata ajali kwa kununua mataili ambayo hayana ubora halafu kuna Waziri anasimamia wizara hii na kuna mamlaka yalisimamia na wanakuja leo mbele yetu kuja kuomba pesa tena” Luhaga Mpina