TAKUKURU MANYARA YAOKOA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 300

.

Afarah Suleiman, Babati – Manyara.

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Manyara imeokoa zaidi ya shilingi milioni 300 kwa kipindi cha january hadi march mwaka huu, ambazo zilipangwa kwenda kinyume na matumizi sahihi ya fedha hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Manyara, Adam Mbwana, amesema wameokoa zaidi ya shilingi milioni 260 kutoka kwa wawekezaji waliopangisha katika hifadhi ya wanyamapori burunge ambayo ni fedha ya kodi ya kupangisha katika hifadhi inayopaswa kugawanya kwa vijiji husika.

katika hatua nyingine amesema katika kipindi hicho TAKUKURU mkoa wa manyara ilipokea malalamiko 105 yaliyopokelewa na kati ya hayo malalamiko 78 yalihusu rushwa , 27 hayakuhusu rushwa na kesi 15 zilifunguliwa mahakamani ambapo kesi 8 zinaendelea na mahakamani.

Aidha, walifanikiwa kudhibiti hatari ya usalama wa vifo kwa wagonjwa wa kata ya Dongobesh wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, baada ya kutengenezwa kwa gari la kubebea wa gonjwa wa Zahanati ya kata hiyo kutokana na kukaa kwa kipindi kirefu bila huduma bora ya kufikisha wagonjwa hospitali

Ni baada ya wananchi wa kata hiyo kupeleka malalamiko yao kwa TAKUKURU kuona gari lipo lakini kila wakilihitaji kwaajili ya kubebea wagonjwa wao hujibiwa na wahusika kuwa ni bovu na hakuna jitihada zozote za kulitengeneza.

TAKUKURU imewataka Wananchi mkoani Manyara kuendelea kutoa taarifa wanapobaini viashiria vyovyote vya rushwa, ili hatua kali zichukuliwe kwa wahusika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *