Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sixtus Mapunda amewataka Wakuu wa idara na taasisi mbalimbali Nchini kutumia Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere kuwapa mafunzo na elimu ya Uongozi ya uwajibikaji watumishi na wafanyakazi wao Ili kuondokana na changamoto za migogoro na kuongeza utendaji kazi maofisini.
Akizungumza Mara baada ya kufunga Mafunzo ya Uongozi Kwa viongozi Kutoka Taasisi mbalimbali hapa Nchini Katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Kibaha Kwa Mfipa Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sixton Mapunda akiwa Mgeni Rasmi amesema shule hiyo Ina miundo mbinu Bora na elimu inayotolewa ni msaada mkubwa kwa watumishi na wafanyakazi nchini.
Alisema kuna uzembe wa utendaji na changamoto baina ya wafanyakazi hutokea kwasababu ya ukosefu elimu ya Uongozi ya uwajibikaji kazini hivyo wanapopata mafunzo hayo kila mmoja hujitambua na migogoro kazini inakwisha.

“Kwa zile Taasisi za Halmashauri na Wilaya zote nchini kuanzia kada za walimu wa taaluma, Watumishi wa sekta mbalimbali na wasimamizi wa maadili wote nawashauri waje wapate elimu ya mafunzo ya Uongozi katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere ili waweze kuongeza wigo wa elimu zao hata kama tayari wako maofisini kwani elimu haina mwisho” alisema Mapunda.
Amesema ya Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere ina kuziba ombwe la changamoto elimu ya Uongozi kwa Viongozi kazini katika nyanja za kada zote nchini hivyo taasisi na idara mbalimbali za serikali na binafsi zitumie kuendeleza watumishi wao.
Aidha Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere John Baytani amesema Mafunzo hayo Kwa viongozi hao yametolewa kwa kuzingatia ubora bapo wamejifunza mambo mbalimbali ikiwamo Afya ya akili na namna ya kuongoza rasilimali Watu ambapo wametoka wakiwa wameiva.

Baytani alisema Wahitimu Hao 21 ambao wamepatiwa Mafunzo ya Uongozi ni Vijana Kutoka Taasisi mbalimbali Nchini yatakuwa chachu Kwa wengine kuona namna ya kwenda kujifunza na kupata Elimu hiyo ya Uongozi shuleni hapo.
Naye mwakilishi wa wanafunzi hao waliohitimu Mafunzo ya Vijana father John Ntwale kutoka Jimbo la Mwanza amesema wakitoka hapo wataenda kuyafanyia kazi Mafunzo waliyoyapata hasa Kwa Kuwa na mshikamano dhabiti.
Father Ntwale amaesema kuwa mafunzo hayo yamewaongezea ufahamu wa uongozi na yamewafungua na kuwapa mbinu kama viongozi za kutawala hisia pindi wanapokuwa na ghadhabu kama binadamu humu amewaomba watanzania wote pindi watakapopata fursa wakasome shuleni hapo na amtunda watayaona.

Aidha amewataka viongozi wa dini wote wajitokeze wasome mafunzo haya yapo hayana mipaka yanasaidia kuibadilisha jamii nzima viongozi wote tungane katika kuleta mabadiliko ya kweli na siyo kwa viongozi wa dini pekee.
“tumejifunza namna ya kutawala hisia na kuwa watulivu tatizo la kupata mfadhaiko na sonona yamekithiri duniani kote, ukiwa kiongozi changamoto zipo ila ufundi wa kiongozi ni kuzivuka na kuzikabili changamoto hizo” amasema Father Ntwale.