TARURA KUTUMIA TILIONI 1.18 KUIMARISHA BARABARA WILAYANI

Wakala Wa Barabara Nchini (TARURA), imepanga kutumia Bajeti ya Shilingi Tilioni 1.18 katika kuimarisha Barabara Wilayani kwa mwaka 2025 – 2026.

Hayo yamesemwa Leo Aprili 22, 2025 Bungeni Jijini Dodoma, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Zainab Katimba wakati akijibu swali la Mbunge Stanslaus Mabula aliyeuliza Je, kuna mpango gani kuiongezea fedha TARURA ili kujenga barabara za ndani ikiwemo ya Mkuyuni – Mahina hadi Nyakato.

Amesema Serikali imeendelea kuiongezea bajeti TARURA kutoka shilingi bilioni 275.03 katika mwaka 2020/21hadi shilingi bilioni 886.30 mwaka 2024/25.

Barabara ya Mkuyuni – Mahina –Nyakatoyenye urefu wa kilomita 11.02 imeshafanyiwa usanifu wa kina ambapo makadirio ya kuijenga kwa tabaka la lami   ni shilingi bilioni 22. Ujenzi wa barabara hiyo kwa urefu wa kilomita mbili unatarajiwa kuanza mwaka 2025/26.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *