SIMBU AIPAISHA BENDERA YA TANZANIA KIMATAIFA

Mwanariadha wa Tanzania, Alphonce Simbu ameipaisha Tanzania anga za kimataifa kwa kushika nafasi ya pili kwenye mbio za Boston Marathon na kupata zawadi ya Dola za Marekani 75,000.

Ushindi wa Simbu umekuja baada ya kushiriki mbio za kilomita 42 zilizoshirikisha Wanariadha wa Mataifa mbalim Ali Duniani na kumaliza katika nafasi hiyo kwa muda wa saa 2:05:04.

Mshindi wa kwanza katika mashindano hayo alikuwa ni Mkenya, John Korir ambaye alitumia saa 2:04:45, na kufanikiwa kuchukua zawadi ya Dola 150,000.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *