Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

WANANCHI WAIBURUZA FOUNTAIN GATE FC

Klabu ya Soka ya Yanga wameendeleza rekodi yao ya ushindi na kuzidi kujichimbia kileleni kufuatia ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Fountain Gate FC.

Katika Mchezo huo uliopigwa uwanja wa Tanzanite Kwaraa uliopo Babati Mkoani Manyara, magoli ya Yanga SC yamepatikana kupitia kwa Clement Mzize aliyefunga mawili na ambaye sasa anafikisha jumla ya mabao 13 kwenye msimamo wa ufungaji bora wa Ligi Kuu bara.

Mabao mengine yamefungwa na Aziz Ki na Clatous Chama, yakiifanya Yanga SC sasa kufikisha pointi 70 baada ya mechi 26, wakicheza mechi nne zaidi ya Simba SC anayeshika nafasi ya pili kwa pointi 57.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *